WALIMU WENYE ULEMAVU WAELEKEZA KILIO CHAO SERIKALINI

Walimu wenye ulemavu wamesema wamekuwa wakikaliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo miundombinu kutokuwa rafiki kwao. Wakizungumza leo jijini Dodoma katika kongangano lililowakutanisha walimu wenye ulemavu Tanzania, wamesema hali hiyo imepelekea kutofanya kazi zao kwa ufanisi unatakiwa. Aidha, wameiomba serikali kuwasaidia walimu wenye ulemavu kwa kupunguza changamoto zinazowakabili ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa